Samia Suluhu
1,820 posts
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. President of the United Republic of Tanzania
Dodoma, Tanzania
Joined June 2014
- Mwaka huu Tanzania na Singapore tunaadhimisha miaka 45 ya uhusiano wetu ambapo kwa upekee leo tumempokea Rais wa Singapore, Mheshimiwa Tharman Shanmugaratnam, Ikulu jijini Dar es Salaam. Hii ni historia na heshima kwa nchi yetu kwani ni mara ya kwanza Rais wa nchi hiyo kutembelea
- Nikihitimisha ziara yangu ya Kitaifa katika Shirikisho la Urusi, leo pamoja na mambo mengine nimepata fursa ya kuhutubia Jukwaa la Biashara kati ya Tanzania na Urusi pamoja na Jukwaa la 29 la Kimataifa la Uchumi la St. Petersburg (SPIEF), ambayo yamekutanisha viongozi, wataalamu
- Ninalishukuru Baraza la Taaluma la Chuo Kikuu cha Urafiki wa Watu wa Urusi (RUDN University) kwa kunitunuku Shahada ya Udaktari wa Heshima (Honoris Causa). Nimepokea heshima hii kwa unyenyekevu mkubwa kwa niaba ya Watanzania wote ambao ndiyo msingi wa mafanikio tunayojivunia na
- Siku ya kwanza ya ziara yangu ya kitaifa katika Shirikisho la Urusi ambapo pamoja na mambo mengine, nimepata heshima ya kukutana na kufanya mazungumzo na Mheshimiwa Rais Vladimir Putin jijini Moscow. Kwa pamoja tumepongeza ukuaji wa biashara kati ya nchi zetu uliofikia asilimia
- Shukrani kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa neema na baraka zake, katika kazi ya kuendelea kuitumikia nchi yetu na watu wake. Nimewasili jijini Moscow, Shirikisho la Urusi ambapo nimeanza ziara ya kitaifa kwa mwaliko wa Mheshimiwa Rais Vladimir Putin.
- Nimeondoka nchini leo kuelekea Shirikisho la Urusi kwa ziara ya Kitaifa kufuatia mwaliko wa Mheshimiwa Rais Vladimir Putin, ikiwa ni ziara ya pili kufanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, baada ya ile ya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, Oktoba 1969. Ziara hii
- Utoaji wa mafunzo kwa Jeshi la Polisi ni moja ya nyenzo zinazoliwezesha kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya kiteknolojia, kiuchumi na kisiasa duniani katika kuimarisha usalama wa raia na mali zao. Ni kwa muktadha huo leo nimefarijika kuhitimisha Mafunzo ya Maafisa na
- Ninawatakia nyote kheri ya Sikukuu ya Eid Al Adha. Tusherehekee kwa moyo wa amani na upendo, huku tukiwakumbuka ndugu zetu wenye uhitaji, na kuendelea kudumisha utu na ukarimu katika jamii. Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema apokee dua na sadaka zetu na aendelee kulibariki Taifa
- Nimepokea kwa masikitiko taarifa ya kifo cha Bi. Khadija Said Salmin, Mtangazaji wa Habari wa Kwanza Mwanamke nchini Tanzania, kilichotokea leo mkoani Dar es Salaam. Tutamkumbuka na kumuenzi Bi. Khadija kwa uthubutu, weledi, nidhamu, umahiri katika kazi na mchango wake, kama













































