user avatar
Faustine Ndugulile
@DocFaustine
Doctor. Parliamentarian. Fmr Minister ICT. Fmr Deputy Minister of Health. Passionate about Sports, ICT & Global Health. WHO AFRO Regional Director-Elect
Tanzania
Joined March 2009
Posts
  • user avatar
    Nimepokea uamuzi wa Mhe Rais kwa unyenyekevu mkubwa. Ninamshukuru sana JPM kwa kunipa fursa ya kuhudumu katika Serikali yake. Nawashukuru sana @umwalimu na watendaji wote kwa ushirikiano walionipatia. Mafanikio ya sekta ni makubwa sana. Namtakia kila la kheri NW ajaye Dkt Mollel.
  • user avatar
    Namshukuru sana Mhe Rais Samia Suluhu Hassan kwa kunipa fursa ya kuhudumu katika Serikali yake. Nawashukuru Wizara na Taasisi zake kwa ushirikiano walionipa. Nashukuru wadau wa TEHAMA kwa ushirikiano mlionipa. Hongera sana Mhe Dkt Ashatu Kijaji kwa kuteuliwa. Kazi Iendelee
  • user avatar
  • user avatar
    Tunawashukuru nyote kwa kushirikiana nasi kwa hali na mali tangu msiba wa Baba yetu Gabriel Sengo Ndugulile utokee tarehe 18.07.2020 Kigamboni hadi kuzikwa kwake Nzega tarehe 24.07.2020. Itoshe kusema ASANTENI SANA. Kama familia tumefarijika salama kwa upendo wenu.
  • user avatar
    Nahitaji posters na flyers kwa ajili ya kampeni za uchaguzi. Nawakaribisha graphic designers kunitumia sampuli zikiwa na picha, jina langu na kaulimbiu kwa njia ya DM. Nitawasiliana TU kwa maongezi zaidi na wale ambao kazi zao zitakuwa za viwango na ubunifu wa juu. Karibuni.
  • user avatar
    SHUKRANI SANA "WAJUMBE" Kwa unyenyekevu mkubwa napenda kuwashukuru sana WAJUMBE wa Halmashauri Kuu CCM (T), Kamati Kuu na Kamati za Siasa waliojadili na kupitisha jina langu kuwa Mgombea wa Ubunge Jimbo la… instagram.com/p/CEHZtKMAAKW/…
  • user avatar
    Tanzania bado tuko nyuma sana katika biashara mtandao. Tunahitaji kukuza na kuilea e-commerce. Vijana wengi wamejiajiri kupitia mfumo huu. Kuanza kutoza kodi mapema kutadumaza mfumo huu na kuua ajira nyingi. Nguvu ielekezwe katika kuimarisha usalama na imani kwenye biashara hii.
  • user avatar
    Leo nimepata fursa ya kukabidhi rasmi ofisi kwa Naibu Waziri wa Afya. Nimpongeza Dkt Mollel kwa kuteuliwa na kumshukuru sana Mhe Waziri Ummy kwa ushirikiano alionipa. Nimemshukuru Rais Dkt Magufuli kwa imani yake kwangu katika kipindi chote nilichohudumu kwenye nafasi hii.
  • user avatar
    Eid Mubarak kwako na familia yako. Tusherekee kwa amani na utulivu huku tukichukua tahadhari zote tunazoshauriwa na wataalamu wa afya kuhusu ugonjwa wa Covid-19. Nawatakia sikukuu njema. #eidmubarak #Eid2020
  • user avatar
    Suala la taa kuzima Uwanja wa Benjamin Mkapa ni aibu kubwa sana kwa nchi yetu. Maswali ya kujiuliza: 1. Je hatufanyi ukaguzi wa mifumo kabla ya mechi? 2. Je, hatuna mifumo ya dharura yanapotokea majanga? 3. Fedha za mgao wa uwanja zinaenda wapi?
  • user avatar
    Mengi yamesemwa kuhusu Hayati Benjamin Mkapa, nami niseme moja. mwaka 2004 nikiwa Ofisa ndani ya Wizara ya Afya tuliazimia kuanzisha mpango wa kutoa dawa za kurefusha maisha kwa watu wanaoishi na VVU nchini (ARVs).… instagram.com/p/CDNruylAOjW/…
  • user avatar
    Kuna taharuki kubwa kuhusu uhaba wa vidonge vya Vitamin C kwa baadhi ya maeneo hapa nchini. Sisi kama wataalamu wa afya, tunashauri zaidi watu watumie matunda kama machungwa, malimao, ndimu, mananasi na mapapai nk. Vidonge ni mbadala pale hakuna matunda na mboga zenye Vit C.
  • user avatar
    Tupuuze taarifa za uzushi zinazosambazwa kuhusu afya yangu. Niko mzima kabisa na ninaendelea na majukumu yangu. Pole nyingi kwa walioguswa na taarifa za uzushi. Disregard the FAKE NEWS circulating that I am unwell. I am Ok and busy with my usual routine. Keep well and safe
  • user avatar
    Kila la kheri Yanga. Nashukuru kwa kuchagua Kigamboni kuwa sehemu ya kuweka kambi yenu.