Love is the first universal language,then follows music and then football.
It's time for football fans to speak their language globally.
May it be entertaining.
Good evening fam.
Nguvu yako na uimara wako ndio utakufanya uone maisha ni rahisi au magumu.Watu wenye nguvu hupambana na changamoto bila kuchoka wala kurudi nyuma.
Tunaomba Mungu nguvu ya kuhimili mikiki,hatuombi urahisi wa maisha.
May this september be a blessed one.
Good morning fam.
Yawezekana ni mazoea au ni mfumo wa maisha tulioukuta,pesa tamu zaidi ni ile uliyoipambania kwa jasho lako na ndio huwa inaheshimiwa zaidi na kufanya maendeleo.
Imani inasema easy money disappears the way it came.
Wachache sana huwa wanafanya mambo tofauti.
Good morning fam.
Unachokitoa mdomoni mwako kinawakilisha kilicho kichwani mwako,na ndio tunachokupimia ubora wa akili yako.
Kwa bahati mbaya hadhi ya mtu huwa inahadaa akili na kujiona yeye ni bora kuliko wengi ko anaongea bila kufikiri,unaweza onekana kichaa au mwenye hekima.
Good morning fam.
Huruma sio upendo lakini tuna uhakika kuwa anayekupenda ni lazima awe na huruma na wewe.
Kuna vitu mtu anaweza akataka kwako na vinakuharibia maisha, anasema anakupenda na wewe unaamini,akupendae hawezi kuharibu maisha yako mana ni yake pia.
Don't love blindly.
Good morning fam.
Tafuta pesa kwa nguvu mpaka ufanikiwe kuzipata,pesa ikupe kujiamini.
Ikikupa jeuri basi inaweza kuwa ni anguko lako.Ugumu wa pesa sio kuipata bali ni kuifanya iendelee kuwa yako.Wengi walipata pesa ila wakarudi kwenye umasikini na hawajanyenyuka tena.
Good morning fam.
Watu hawawezi kuelewa unachopitia mpaka pale na wao watakapopitia kile ulichopitia. Na ndio maana ni ngumu kumshauri mtu aliye kwenye matatizo ambayo wewe hujayapitia,majibu yote huwa nayo mlengwa ni vile tu anahitaji support ya kile ambacho tayari anajua.
Good morning fam.
Kulingana na uhalisia wa maisha,watu wanatumika,hakuna upendo.
Boss anaangalia faida yake,sio utu wala afya yako.Mke anaangalia unachotoa mezani,sio unapata kwa tabu kiasi gani.Mpenzi anataka apendeze kama rafiki yake hata kama kipato chako kidogo.
Jipende.
Good morning fam.
Usijenge ndoto zako juu ya maumivu ya watu wengine,malipo yake itakua ni kuishi bila furaha.
Kila mtu ana kusudi la kuwepo alipo,wewe sio muhim kuliko wengine.
Chagua njia sahihi ya kufika utakako,vilio na manung'uniko ya watu huleta laana hasa vikiwa vya haki.
Good morning fam.
Even the strongest men feel weak when ignored.
Usije fanya kosa la kumnunia na kumpuuzia mpenzi wako,ataenda na maji.
Mungu aliona upweke wa Adam na akamfanyia msaidizi,yani hakuna kitu utafanya kichukue nafasi ya mtu.Suluhisha ugomvi,usipotezee,utapoteza.
Good morning fam
Don't take it personal,people change.
Iwe kwenye undugu,urafiki au mapenzi ni huwa inaumiza sana mtu uliyedhani ni wako daima kubadilika mazima.
Usijitafutie kasoro wala kujichukia,watu hubadilika tu kwa sababu zao binafsi zilizo nje ya uwezo wako.Endelea kuwa wewe.
Gm friends.
Unaweza kuwa mbinafsi pasipo kujua,ukiwa na uwezo mdogo wa kuwaza mbali unaweza ukawa unafanya mambo kwa ajili yako tu bila kujua kuwa unaathiri kizazi chako kijacho.
Kumbuka kuwa kila kitu ufanyacho kina madhara chanya/hasi kwenye maisha yako.
Fanya maamuzi sahihi.
Good morning
Furaha na amani vimekua bidhaa adimu sana kitaa,kuliko hata pesa,kitu kikiadimika ndio thamani yake inapanda pia.
Unaona ongezeko la comedians kwa sasa? Yani imekua unalipia kupata furaha meaning it's a sad generation.
Kuwa tone la furaha kwenye jamii,amani itakuja.
Gm fam.
Ubora wa mwanaume mara nyingi huwa unaonekana kwenye familia yake,iwe alipozaliwa au kwa mke wake,mara nyingi wanaume huwa wanajali watu wao kuliko kujijali wao hivyo huwezi mthaminisha mwanaume kwa kumuangalia yeye bali watu wake.
We should love ourselve first
Good morning fam.