Mungu anakupenda kabisa! Upendo wake hauna mipaka na hauenendi na hali. Upendo wa mungu umejidhihirisha kupitia kwa Yesu kristo. Huyu mungu anayetupenda aweza dhihirika, Yeye ni wa kweli na haitaji chochote ila wewe mwenyewe ushuhudie Upendo wake na ugundue sababu ya maisha Yako katika mahusiano baina Yako na Yeye.
Dhambi zetu na matendo yetu ya uchoyo hayamfanyi mungu kuacha kutupenda. Ata akawa mtu kupitia kwa Yesu na akatoa uhai wake kwa ajili yetu. Akachukua nafasi yetu katika msalaba akibeba kila madhara ya dhambi mwenyewe.Yesu akafa-lakini akafufuka akawa hai Tena. Ametupa amani na mungu uhusiano wa kipekee naye. Kupitia Imani kwa Yesu tunaweza shuhudia Upendo wa mungu kila siku, gundua malengo yetu na kuwa na uzima wa milele baada ya kifo.
Mungu tayari ashafanya kila kitu kutuonyesha jinsi gani anavyotupenda. Kupitia kwa Yesu kristo anatupa hitimizo na uzima wa milele. Tunaweza kuongea na mungu Moja kwa moja-twa iita “maombi”-kuomba msamaha kwa kuishi maisha yetu bila Yeye. Twaweza chagua kuishi na mungu kwa kuamini Yesu kristo kutoka Sasa na kuendelea. Utaamuaje?
Je, ungependa kufanya hivyo leo?
Kuanza uhusiano wako binafsi na Mungu huyu mwenye upendo ni bure, ni rahisi kabisa, na itabadilisha maisha yako.
You will be redirected to your country's page...