Maria Chudnovsky
| Maria Chudnovsky | |
|---|---|
| Picha MariaChudnovsky 2011 | |
| Tarehe ya kuzaliwa | Januari 6, 1977 |
| Mahali pa kuzaliwa | St. Petersburg, Russia |
| Uraia | Israeli-American |
| Taasisi | Princeton University |
| Idara | Hisabati |
| Cheo | Profesa |
| Elimu | Shahada ya Uzamivu |
| Shahada ya kwanza | |
| Shahada ya pili | |
| Shahada ya uzamivu | 2003 |
| Mada ya tasnifu | |
| Mwaka wa uzamivu | 2014 |
| Mshauri wa uzamivu | |
| Eneo la utafiti | graph theory |
| Michango mashuhuri | |
| Machapisho | |
| Tuzo | Brilliant 10 |
| Tovuti | |
Maria Chudnovsky (amezaliwa Januari 6, 1977) ni mwanahisabati wenye asili ya Israeli na Marekani anayefanya kazi katika nadharia ya grafu na uboreshaji wa pamoja (graph theory and combinatorial optimization).[1] Yeye ni Mshirika wa MacArthur_Fellows_Program MacArthur kwa mwaka 2012.[2]
Elimu na Kazi
[hariri | hariri chanzo]Chudnovsky ni profesa katika idara ya hisabati katika Chuo Kikuu cha Princeton. Alikulia nchini Urusi (alisoma shule ya Saint Petersburg Lyceum 30) na Israeli, akisoma katika Technion, [3] na baadae kupokea Shahada ya Uzamivu mwaka wa 2003 kutoka Chuo Kikuu cha Princeton chini ya usimamizi wa Paul Seymour. Baada ya utafiti wa Shahada ya uzamivu katika Taasisi ya Hisabati ya Clay, alikua profesa msaidizi katika Chuo Kikuu cha Princeton mnamo 2005, na kuhamia Chuo Kikuu cha Columbia mnamo 2006. Kufikia 2014, alikuwa Profesa wa Familia ya Liu wa Uhandisi wa Viwanda na Utafiti wa Uendeshaji huko Columbia. Alirudi Princeton kama profesa wa hisabati mwaka 2015.[4]
Tuzo na Heshima
[hariri | hariri chanzo]Mnamo 2004, Chudnovsky jina lake lilitajwa kwenye "Brilliant 10" na gazeti moja lijulikanalo kama Popular Science magazine kazi yake ya graph theorem ndiyo iliyomtambulisha na kujumuishwa kwenye orodha hii maarufu pamoja na washiriki wenza mwaka 2009.[5]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ https://web.math.princeton.edu/~mchudnov/cv.pdf
- ↑ https://web.archive.org/web/20121002000603/http://bigstory.ap.org/article/2012-macarthur-foundation-genius-grant-winners#overlay-context=users/rjagodzinski
- ↑ https://www.claymath.org/library/annual_report/ar2005/05report_chud.pdf
- ↑ https://web.archive.org/web/20121002000603/http://bigstory.ap.org/article/2012-macarthur-foundation-genius-grant-winners#overlay-context=users/rjagodzinski
- ↑ https://www.ams.org/notices/201011/rtx101101475p.pdf